• HABARI MPYA

    Tuesday, January 20, 2026

    SIMBA SC YAMTAMBULISHA BEKI MPYA MUIVORY COAST ALIKUWA ANACHEZA ABU DHABI


    KLABU ya Simba imemtambulisha beki wa kati, Ismaël Olivier Touré (28) kujiunga na Wekundu hao wa Msimbazi akitokea FC Baniyas ya Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
    Beki huyo anayeweza kucheza kama kiungo wa ulinzi pia anakwenda Simba kuungana tena na kocha Steven Robert 'Steve' Barker ambaye alifanya naye kazi Stellenbosch FC ya Afrika Kusini kabla ya khamia UAE.
    Mbali na Baniyas na Stellenbosch FC, timu nyingine ambazo Touré amechezea ni Marumo Gallants FC ya Afrika Kusini pia, ASEC Mimosas, AFAD-Plateau na ES Bingerville zote za kwao, Ivory Coast.
    Anakuwa mchezaji mpya wa tatu mpya kwa Simba SC dirisha hili dogo baada ya beki wa kushoto mzawa, Nickson Clement Kibabage (25) kutoka Singida Black Stars ya nyumbani na winga wa kushoto Msenegal, Libasse Gueye (22) kutoka Teungueth FC ya kwao. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAMTAMBULISHA BEKI MPYA MUIVORY COAST ALIKUWA ANACHEZA ABU DHABI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top