WENYEJI, Manchester City jana waliiibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya West Ham United FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mabao ya Man City katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland dakika ya tano na 69 na kiungo Mholanzi, Tijjani Reijnders dakika ya 38.
Kwa ushindi, Man City inafikisha pointi 37 ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mchi 17 sasa, wakati West Ham United wanabaki na pointi zao 13 za mechi 17 nafasi ya 18.



.png)
0 comments:
Post a Comment