Mabao ya Msumbiji yamefungwa na mshambuliaji wa Mestre ya Italia, Faisal Bangal dakika ya 37, winga wa Sporting Lisbon ya Ureno, Geny Cipriano Catamo dakika ya 42 kwa penalti na beki wa kulia wa Santa Clara ya Ureno pia, Diogo Calila dakika ya 42.
Kwa upande wao Gabon mabao yao yamefungwa na mshambuliaji wake mkongwe na Nahodha wake, Pierre-Emerick Emiliano François Aubameyang ambaye kwa sasa anachezea Marseille ya Ufaransa dakika ya 45’+5 na beki wa kati wa Aris Limassol ya Cyprus, Alex Yowan Kevin Moucketou-Moussounda dakika ya 76.
Kwa ushindi huo, Msumbiji inakusanya pointi tatu za kwanza katika mchezo wa pili kufuatia kuchapwa 1-0 na Ivory Coast katika mchezo wa kwanza, wakati Gabon inakamilisha mechi mbili bila hata pointi moja kufuatia kufungwa na Cameroon 1-0 pia kwenye mchezo wa kwanza.
Baadaye Saa 5:00 usiku mechi tamu kabisa ya Kundi hilo itafuatia kati ya Tembo wa Ivory Coast na Simba Wasiofungika wa Cameroon Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech.



.png)
0 comments:
Post a Comment