WINGA wa zamani wa Yanga SC, Chico Ushindi Wakubanza amefariki dunia leo kwao, Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa ana umri wa miaka 29.
Hadi umauti unamkuta, Chico alikuwa mchezaji wa klabu ya Jeunesse Sportive Groupe Bazano, maarufu kama JS Groupe Bazano ya Lubumbashi aliyojiunga nayo Oktoba 9 akitokea AS Vita ya Kinshasa.
Chicho alijiunga na Yanga katika dirisha dogo Januari 16, mwaka 2022 kwa mkopo akitokea TP Mazembe ambayo ilimuibua CS Don Bosco, zote za Lubumbashi.
Hata hivyo, mwisho wa msimu licha ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Chico alirejeshwa Mazembe Agosti 5 na Agosti 20 aliuzwa kwa mkopo Nejmeh SC ya Lebanon alikocheza kwa miezi miwili tu.
Aliporejea Mazembe Oktoba 21 mwaka 2022 akarudishwa kwa mkopo CS Don Bosco dirisha dogo Januari 1, 2023 ambako alicheza hadi Juni 30 mwaka 2024 mkopo wake ulipoisha akarejea tena Mazembe ambako mkaaba wake ulimalizika Februari 4 mwaka 2025.
Mei 6 alikwenda Kinshasa kujiunga na AS Vita Club, ambakom mambo hayakumuendea vizuri na Oktoba 9 akarudi Lubumbashi kujiunga na JS Bazano.
Mei 6 alikwenda Kinshasa kujiunga na AS Vita Club, ambakom mambo hayakumuendea vizuri na Oktoba 9 akarudi Lubumbashi kujiunga na JS Bazano.
Chico pia amewahi kuchezea timu ya taifa ya DRC na kumbukumbu yake nzuri ni alipoiwezesha kufika Robo fainali ya CHAN kwa kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya jirani zao, Kongo-Brazaville mechi ya ufunguzi ya Kundi B Uwanja wa Japoma Jijini Douala nchini Cameroon.
Hata hivyo, Chico aliumia na kukosa mechi zilizofuata za kundi hilo dhidi ya Libya iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na Niger ambayo DRC ilishinda 2-1 na kwenda Robo Fainali ambako walitolewa na wenyeji, Cameroon kwa kufungwa 2-1.
Mungu ampumzishe kwa amani Chico Ushindi. Amin.








.png)
0 comments:
Post a Comment