TIMU ya Misri imetoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) usiku wa jana Uwanja wa Adrar mjini Agadir nchini Morocco.
Mshambuliaji wa Yanga SC, Prince Dube Mpumelelo alianza kuifungia The Warriors dakika 20, kabla ya The Pharaohs kuzinduka kwa mabao ya washambuliaji wake wanaocheza England, Omar Khaled Mohamed Abdelsalam Marmoush wa Manchester City dakika ya 64 na Mohamed "Mo" Salah Hamed Mahrous Ghaly wa Liverpool dakika ya 90’+1.
Ikumbukwe mchezo mwingine wa kwanza wa Kundi B jana Afrika Kusini ilishindi 2-1 dhidi ya jirani zao, Angola Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech.
Mabao ya Bafana Bafana yalifungwa na winga wa Orlando Pirates, Oswin Reagan Appollis dakika ya 21 na mshambuliaji wa Burnley ya England, Lyle Brent Foster dakika ya 79, wakati la Palancas Negras limefungwa na Manuel Luís da Silva Cafumana anayecheza kwa mkopo Kocaelispor ya Uturuki kutoka Maccabi Haifa ya Israel dakika ya 35.



.png)
0 comments:
Post a Comment