WENYEJI, JKT Tanzania wametoa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, JKT Tanzania inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 10 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu mbele ya Pamba JIji FC yenye pointi 15 za mechi nane.
Kwa upande wao Mtibwa Suga TV baada ya sare ya leo wanafikisha pointi 10 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya sita kwenye Ligi ya timu 16.



.png)
0 comments:
Post a Comment