• HABARI MPYA

    Thursday, December 11, 2025

    MADUEKE AFUNGA MAWILI, ARSENAL YASHINDA 3-0 UBELGIJI LIGI YA MABINGWA


    TIMU ya Arsenal ya England jana iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Club Brugge katika mfululizo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Jan Breydel mjini huko Sint-Andries, Bruges, Ubelgiji. 
    Mabao ya Arsenal yalifungwa na winga wa Kimataifa wa England, Chukwunonso Azuka Tristan ‘Noni’ Madueke mwenye asili ya Nigeria mawili dakika ya 25 na 47, wakati linguine limefungwa na mshambuliaji Mbrazil, Gabriel Martinelli dakika ya 56.
    Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi ya timu 36 Bora‎ ikiizidi pointi moja Bayern Munich ya Ujerumani, wakati Club Brugge inabaki na pointi zake nne nafasi ya 31 baada ya wote kucheza mechi sita.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MADUEKE AFUNGA MAWILI, ARSENAL YASHINDA 3-0 UBELGIJI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top