• HABARI MPYA

    Monday, December 22, 2025

    WENYEJI MOROCCO WAANZA VYEMA AFCON 2025


    WENYEJI, Morocco wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Comoro katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.
    Mabao ya Simba wa Atlasi katika mchezo huo wa ufunguzi yalifungwa na winga wa Real Madrid, Brahim Abdelkader Díaz dakika ya 55 na mshambuliaji wa Olympiacos ya Ugiriki, Ayoub El Kaabi dakika ya 74.
    Morocco ingeweza kuondoka na ushindi mpana zaidi kama si kipa wa Comoro, Yannick Pandor anayedakia  RC Lens ya Ufaransa kuokoa penalti ya Soufiane Rahimi dakika ya 10‎ tu ya mchezo huo.
    Sherehe za ufunguzi zilifana zikiwahusisha Rais wa FIFA, Giannis Infantino, CAF, Dk. Patrice Motsepe na Prince Moulay Abdellah wa Morocco. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENYEJI MOROCCO WAANZA VYEMA AFCON 2025 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top