• HABARI MPYA

    Tuesday, December 09, 2025

    MABINTI WA TANZANIA WATWAA UBINGWA WA SHULE ZA CECAFA


    TIMU ya Wasichana ya Tanzania imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Ubingwa wa Shule za Afrika kanda ya CECAFA baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Ethiopia kufuatia sare ya bila mabao mchana wa leo Uwanja wa FUFA Kadiba, Mengo, Rubaga Jijini Kampala nchini Kampala, Uganda.
    Kwa ushindi huo, mabinti wa Tanzania wamejikatia tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika za Mashindano hayo yanayohusisha wanafunzi wa umri chini ya miaka 15.
    Wenyeji, Uganda wamemaliza nafsi ya tatu upande wa wasichana baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burundi mapema asubuhi hapo hapo Uwanja wa FUFA Kadiba, Mengo, Rubaga Jijini Kampala.
    Mwaka jana Tanzania ilikuwa bingwa wa michuano hiyo ya CECAFA upande wa wavulana na kwenda kutwaa na ubingwa, lakini mwaka huu wameambulia nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Burundi leo Uwanja wa St. Mary's-Kitende, Wakiso, Barabara ya Entebbe, Uganda. 
    Wenyeji, Uganda wametwaa ubingwa upande wa wavulana baada ya kuifunga Ethiopia kwa penalti 3-1 kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa St. Mary's-Kitende, Wakiso, Barabara ya Entebbe, Uganda. 
    Pamoja na kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Shule za Afrika ukanda wa CECAFA kwa wanafunzi chini ya umri wa miaka 15 leo Jijini Kampala nchini Uganda — Tanzania pia imetoa Mfungaji Bora ambaye ni Hajra Mawanja na Kipa Bora, Rukia Suleiman.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABINTI WA TANZANIA WATWAA UBINGWA WA SHULE ZA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top