MISRI imekuwa timu ya kwanza kufuzu Hatua ya Mtoano, 16 Bora baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Afrika Kusini usiku huu katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 Uwanja wa Adrar mjini Agadir nchini Morocco inakoendelea michuano hiyo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Refa Pacifique Ndabihawenimana wa Burundi, bao pekee la The Pharaohs limefungwa na mshambuliaji wa Liverpool ya England, Mohamed "Mo" Salah Hamed Mahrous Ghaly dakika ya 45 kwa penalti.
Kwa ushindi huo, Misri inafikisha pointi sita na kujihakikishia kufuzu Hatua ya 16 Bora ikiwa na mechi moja mkononi dhidi ya Angola.
Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ wanabaki na pointi zao tatu baada ya mechi mbili pia kuelekea mechi ya mwisho dhidi ya Zimbabwe yenye pointi moja sawa na Angola.



.png)
0 comments:
Post a Comment