MABAO ya kiungo Muingereza, Jude Bellingham dakika ya 38 na mshambuliaji Mfaransa, Kylian Mbappé dakika ya 86 jana yaliipa Real Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya Sevilla FC katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi 42, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Barcelona ambayo pia ina mechi moja mkononi na leo inacheza na wenyeji, Villarreal Uwanja wa De la Cerámica.
Sevilla baada ya kupoteza mchezo huo inabaki na pointi zake 20 za mechi 17 sasa naafsi ya tisa kwenye La Liga inayoshirikisha timu 20.



.png)
0 comments:
Post a Comment