KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amekabidhi Shilingi Milioni 50 kwa timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kama pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufuzu mara mbili mfululizo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Desemba 3, 2025 jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya Serikali kutambua juhudi na nidhamu ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi katika safari yao ya kufuzu michuano hiyo mikubwa barani Afrika, inayotarajiwa kufanyika Morocco mwaka 2026.



.png)
0 comments:
Post a Comment