TIMU ya Afrika Kusini imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya jirani zao, Angola katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco.
Mabao ya Bafana Bafana yamefungwa na winga wa Orlando Pirates, Oswin Reagan Appollis dakika ya 21 na mshambuliaji wa Burnley ya England, Lyle Brent Foster dakika ya 79, wakati la Palancas Negras limefungwa na Manuel Luís da Silva Cafumana anayecheza kwa mkopo Kocaelispor ya Uturuki kutoka Maccabi Haifa ya Israel dakika ya 35.
Mchezo mwingine wa Kundi B unafuatia usiku huu kati ya Misri na Zimbabwe Uwanja wa Adrar mjini Agadir.



.png)
0 comments:
Post a Comment