• HABARI MPYA

    Monday, December 08, 2025

    TAIFA STARS YAENDA MISRI KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA AFCON


    KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeondoka leo kwenda Misri kuweka kambi ya kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21  hadi Januari 18, mwakani.
    Taifa Stars inayofundishwa na Kocha Muargentina, Miguel Angel Gamondi itakuwa Misri hadi Desemba 18 itakapoondoka kwenda Morocco tayari kwa AFCON ya 35.
    Taifa Stars ambayo inashiriki Fainali hizo kwa mara ya nne baada ya 1980 Nigeria, 2019 Misri na 2023 Ivory Coast — imepangwa Kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia na Uganda.



    Katika Fainali zote zilizotangulia Taifa Stars imekuwa ikitolewa hatua ya makundi - tena bila kushinda mechi hata moja wakitoa sare na kufungwa.
    Mwaka 1980 walifungwa 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri pamoja na Sara ya 1-1 na Ivory Coast, 2019 walifungwa mechi zote, 2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya na 3-0 na Algeria — wakati mwaka 2023 walifungwa mechi moja, 3-0 na Morocco na sare za 1-1 na Zambia na 0-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YAENDA MISRI KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top