KLABU ya Simba imeachana na Kocha iliyemtambulisha kama Meneja Mkuu, Dimitar Nikolaev Pantev baada ya mwezi mmoja tangu awasili kurithi mikoba ya Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini.
Hatua ya Simba kuachana na Mbulgaria huyo inatokana na mwanzo mbaya katika mechi zake mbili za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika ikifungwa nyumbani na ugenini.
Simba SC ilifungwa 1-0 na Angola Petro de Luanda ya Angola katika mchezo wa kwanza Novemba 23 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya kufungwa 2-1 na Stade Malien Novemba 30 Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako nchini Mali.
Ni mchezo huo wa Jumapili waliopoteza uliofanya Bodi ya Simba ikutane katika kikao cha dharula leo kuamua mustakabali wa timu na hatua iliyochukuliwa ni kung’olewa kwa Pantev.




.png)
0 comments:
Post a Comment