• HABARI MPYA

    Saturday, December 13, 2025

    KOCHA UGANDA AUMIZA KICHWA KUKATA WACHEZAJI WAWILI THE CRANES


    KOCHA Mbelgiji wa Uganda, Paul Put anaumiza kichwa kupunguza wachezaji wawili ili kubaki na 28 wa kuunda kikosi cha mwisho cha The Cranes kwa ajili ya Fainali za  Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco.
    Kikosi hicho cha wachezaji 30 kipo Morocco kwa kambi ya mazoezi ya siku 11 Jijini Casablanca kujiandaa na AFCON na kitakuwa na mechi mbili za kirafiki kabla ya kutangazwa kwa kikosi cha mwisho.
    Uganda wamepangwa katika Kundi C la pamoja na Nigeria, Tanzania na Tunisia huku Put akijivunia mseto wa wachezaji chipukizi na wenye uzoefu wa kimataifa.
    Kipa mkongwe Denis Onyango anarejea kama mmoja wa makipa wanne waliotajwa, huku mchezaji chipukizi James Bogere akiitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wakubwa baada ya kuonyesha kiwango chake bora katika Kombe la Dunia la U17 nchini Qatar.
    Safu ys ushambuliaji imeboreshwa kwa kujumuishwa Mato Rogers, ambaye amefunga mabao 15 katika mechi 17 za FK Vardar ya Macedonia Kaskazini msimu huu.
    Put pia amewarejesha Baba Alhassan na Melvyn Lorenzen waliofanya vizuri katika mechi za kirafiki za Uganda za Novemba.
    Orodha ya mabeki inajumuisha Toby Sibbick wa Burton Albion, Jordan Obita, Abdu Azizi Kayondo na Nahodha wa SC Villa, David Owori, huku Khalid Aucho akiendelea kuongoza safu ya kiungo.
    Uganda itafungua kampeni yake ya AFCON dhidi ya Tunisia Desemba 23, kabla ya kucheza na Nigeria na Tanzania kuangalia nafasi ya kusonga mbele kutoka kundi hilo gumu.


    KIKOSI KAMILI CHA UGANDA AFCON 2025:
    Makipa; Salim Omar Magoola (Richards Bay FC, Afrika Kusini), Denis Onyango (Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Alionzi Nafian (Defence Forces FC, Ethiopia) na Charles Lukwago (KCCA FC)
    Mabeki; Toby Sibbick (Burton Albion, England), Elio Caprodossi (Universitatea Cluj, Romania), Jordan Obita (Hibernian FC, Scotland), Rogers Torach (Vipers SC), Abdu Azizi Kayondo (Slovan Liberec, Jamhuri ya Czech), Isaac Muleme (Viktoria Žižkov, Jamhuri ya Czech), Timothy Awany (FC Ashdod, Israel), David Owori (SC Villa) na Hilary Mukundane (Vipers SC).
    Viungo; Kenneth Semakula (Al-Adalah FC, Saudi Arabia), Khalid Aucho (Singida Black Stars, Tanzania), Ronald Ssekingada, APR FC, Rwanda, Bobosi Byaruhanga (Oakland Roots, Marekani) na Baba Alhassan (FCSB, Romania.
    Washambuliaji; Allan Okello (Vipers SC), Melvyn Lorenzen (Muangthong United, Thailand, Travis Mutyaba (CS Sfaxien, Tunisia), Denis Omedi (APR FC, Rwanda), Mato Rogers (FK Vardar, Macedonia Kaskazini), Reagan Mpande (SC Villa), Jude Ssemugabi (Jamus FC, Sudan Kusini), Uchechukwu Ikpeazu (St. Johnstone, Scotland), Steven Mukwala (Simba SC, (Tanzania), James Bogere (Masaka Sunshine FC), Ivan Ahimbisibwe (KCCA FC) na Shafik Nana Kwikiriza (KCCA FC).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA UGANDA AUMIZA KICHWA KUKATA WACHEZAJI WAWILI THE CRANES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top