TIMU za Mali na Zambia zimetoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Kundi A Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 leo Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Mshambuliaji wa Auxerre ya Ufaransa, Lassine Sinayoko alianza kuifungia Mali dakika ya 62, kabla ya mshambuliaji wa Leicester City yaa England, Patson Daka kuisawazishia Zambia dakika ya 90’+2.
Kwa matokeo hayo, wenyeji Morocco wanaendelea kuongoza kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Comoro jana, wakifuatiwa na Mali na Zambia.



.png)
0 comments:
Post a Comment