• HABARI MPYA

    Friday, December 05, 2025

    TIMU ZA UOGELEAJI NA MPIRA WA MEZA ZAKABIDHIWA BENDERA KUELEKEA MASHINDANO YA AFRIKA


    WACHEZAJI wa timu ya taifa ya mchezo wa kuogelea pamoja na ile ya mpira wa meza wamekabidhiwa bendera leo Desemba 5, 2025, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya safari yao kuelekea Angola tarehe 6 Desemba, mwaka huu. Timu hizo zitashiriki Mashindano ya Nne ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 10 hadi 20 nchini humo.
    Akizungumza katika hafla hiyo, Ofisa Michezo Mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Charles Maguzu, aliwataka wachezaji kuhakikisha wanapigania bendera ya taifa.
    “Nendeni mkapambane, mrudi na makombe na medali. Serikali imetoa fedha na mavazi kwa ajili ya safari na maandalizi yenu,” alisema Maguzu.
    Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Henry Tandau, alisema msafara huo utahusisha watu saba, wakiwemo wachezaji watatu, viongozi wawili na makocha wawili.




    Tanzania itawakilishwa na timu mbili ambazo ni timu ya kuogelea yenye wachezaji wawili na timu ya mpira wa meza yenye mchezaji mmoja,” alifafanua Tandau.
    Naye Meneja wa timu hizo, ambaye pia ni Afisa Michezo wa BMT, Halima Bushiri, alisema maandalizi yamekamilika na timu imejipanga kikamilifu kupambana na kurejea na ushindi.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU ZA UOGELEAJI NA MPIRA WA MEZA ZAKABIDHIWA BENDERA KUELEKEA MASHINDANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top