TIMU ya Liverpool FC jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
Mabao ya Liverpool FC yalifungwa na washambuliaji wake wapya, Msweden mwenye asili ya Eritrea, Alexander Isak dakika ya 56 na Hugo Ekitiké mwenye asili ya Cameroon dakika ya 66, wakati la Tottenham Hotspur limefungwa na mshambuliaji Mbrazil, Richarlison dakika ya 83.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 29 na kusogea nafasi ya tano ikizidiwa tu wastani wa mabao na Chelsea baada ya wote kucheza mechi 17, wakati Tottenham Hotspur inabaki na pointi zake 22 za mechi 17 pia nafasi ya 13.



.png)
0 comments:
Post a Comment