• HABARI MPYA

    Saturday, December 13, 2025

    NIGERIA YATEUA WACHEZAJI 28 KIKOSI CHA MWISHO AFCON 2025


    KOCHA wa Nigeria, Eric Chelle ametaja kikosi cha wachezaji 28 wazuri kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco, akiwajumuisha washambuliaji nyota Victor Osimhen na Ademola Lookman.
    Super Eagles, walioshika nafasi ya pili katika AFCON iliyopita, watafungua kampeni yao ya Kundi C mnamo Desemba 23 kwa kumenyana na Tanzania, kabla ya kukabiliana na Tunisia na baadaye Uganda kukamilisha mechi zao za kundi kutafuta nafasi ya kufuzu Hatua ya Mtoano.
    Washindi wawili wa kila Kundi watafuzu moja kwa moja hatua ya Mtoano wakiungana na timu nyingine nne kati ya sita zilizoshika nafasi ya tatu kwa wastani mzuri zaidi kwenye makundi yote sita.
    ikiongozwa na Osimhen anayechezea Galatasaray ya Uturuki na Lookman wa Atalanta ya Italia, Nigeria inakwenda AFCON ikipewa nafasi kubwa ya kufika mbali kwenye michuano hiyo.
    Mara ya mwisho Nigeria ilitwaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 ikiifunga Burkina Faso 1-0 katika Fainali bao la Sunday Mba dakika ya 40 Uwanja wa FNB Jijini Johannesburg, Afrika Kusini Februari 10, wakati mwaka jana ilifika Fainali pia na kufungwa 2-1 na wenyeji, Ivory Coast Februari 1 Uwanja wa Alassane Ouattara Jijini Abidjan. 
    Kwa kikosi cha Chelle kinachojivunia uzoefu, kina na vipaji vya hali ya juu, matarajio ni makubwa huku Super Eagles wakijiandaa kwa mechi ya kujipasha joto dhidi ya Misri mnamo Desemba 16 kabla ya kuruka hadi Fes kwa ajili ya mechi zao za makundi.


    KIKOSI KAMILI CHA NIGERIA AFCON 2025
    Makipa; Stanley Nwabali (Chippa United, South Africa), Amas Obasogie (Singida Black Stars, Tanzania) na Francis Uzoho (Omonia, Cyprus).
    Mabeki; Calvin Bassey (Fulham, England), Semi Ajayi (Hull City, England), Bright Osayi-Samuel (Birmingham City, England), Bruno Onyemaechi (Olympiacos, Ugiriki), Chidozie Awaziem (Nantes, Ufaransa), Zaidu Sanusi (Porto, Ureno), Igoh Ogbu (Slavia Prague, Jamhuri ya Czech), Ryan Alebiosu (Blackburn Rovers, England).
    Viungo; Alex Iwobi (Fulham, England), Frank Onyeka (Brentford, England), Wilfred Ndidi (Besiktas, Uturuki), Raphael Onyedika (Club Brugge, Ubelgiji), Tochukwu Nnadi (Zulte Waregem, Ubelgiji), Fisayo Dele-Bashiru (Lazio, Italia), Ebenezer Akinsanmiro (Pisa, Italia) na Usman Muhammed (Ironi Tiberias, Israel).
    Washambuliaji; Chidera Ejuke (Sevilla, Hispania), Akor Adams (Sevilla, Hispania), Ademola Lookman (Atalanta, Italia), Samuel Chukwueze (Fulham, England), Victor Osimhen (Galatasaray, Uturuki), Moses Simon (Paris FC, Ufaransa), Paul Onuachu (Trabzonspor, Uturuki), Cyriel Dessers (Panathinaikos, Ugiriki) na Salim Fago Lawal (Istra 1961, Croatia).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIGERIA YATEUA WACHEZAJI 28 KIKOSI CHA MWISHO AFCON 2025 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top