WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na viungo, Yahya Zayd Omary dakika ya 24 kwa penalti, Feisal Salum Abdallah dakika ya 35 na mshambuliaji Mkongo, Jephte Kitambala Bola dakika ya 45’+2.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 12 katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya sita, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake tisa za mechi tisa sasa nafasi ya 12 kwenye Ligi ya timu 16.



.png)
0 comments:
Post a Comment