• HABARI MPYA

    Saturday, December 06, 2025

    MAXIMO AFUTWA KAZI KMC BAADA YA MIEZI MINNE TU


    TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imeachana na kocha Mbrazil, Márcio Máximo Barcellos baada ya miezi minne kutokana na matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
    Maximo alijiunga na TRA Julai 25, mwaka huu lakini ameshindwa kuiweka kwenye nafasi nzuri timu hiyo hadi sasa ikiwa katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya timu 16 kufuatia kuambulia pointi nne tu katika mechi tisa – ikishinda moja, sare moja na kufungwa saba.
    KMC inakuwa klabu ya pili kwa Maximo kufukuzwa nchini baada ya Yanga SC mwaka 2014 kufuatia awali kufanya kazi kwa mafanikio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kati ya mwaka 2006 na 2010 akiiwezesha kufuzu Fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast enzi hizo zikishirikisha timu nane tu.


    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXIMO AFUTWA KAZI KMC BAADA YA MIEZI MINNE TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top