• HABARI MPYA

    Sunday, December 28, 2025

    NIGERIA YAICHAPA TUNISIA 3-2 NA KUTINGA 16 BORA AFCION 2025


    TIMU ya Nigeria imekata tiketi ya kwenda Hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tunisia katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Fez mjini Fez nchini Morocco.
    Mabao ya Super Eagles yalifungwa na  nyota wanaocheza Uturuki, Victor James Osimhen wa Galatasaray, dakika ya 44, Onyinye Wilfred Ndidi wa Beşiktaş dakika ya 50 na Ademola Lookman Olajade Alade Ayoola Lookman wa Atalanta ya Italia.
    Kwa upande wao, Eagles of Carthage mabao yao yalifungwa na mabeki wanaocheza Ufaransa, Montassar Omar Talbi wa Lorient ya Ufaransa dakika ya 74 na Ali El Abdi wa Nice dakika ya 87 kwa penalti.
    Kwa matokeo hayo, Nigeria inafikisha pointi sita kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania kwenye mchezo wake wa kwanza na kusonga mbele Hatua ya 16 Bora ikiwa na mechi moja mkononi dhidi ya Uganda.
    Kwa upande wao, Tunisia ambao mechi ya kwanza waliichapa Uganda 3-1, wanabaki na pointi zao tatu kuelekea mchezo wao wa mwisho dhidi ya Tanzania. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIGERIA YAICHAPA TUNISIA 3-2 NA KUTINGA 16 BORA AFCION 2025 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top