TIMU ya Algeria imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Burkina Faso usiku huu Uwanja wa Moulay Hassan Jijini Rabat nchini Morocco.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Daniel Nii Laryea Ghana, bao pekee la Algeria limefungwana winga wa Al Ahli ya Saudi Arabia, Riyad Karim Mahrez dakika ya 23 kwa penalti.
Kwa ushindi huo, Algeria wanafikisha pointi sita katika mchezo wa pili, wakati Burkina Faso inabaki na pointi zake tatu sawa na Sudan, mbele ya Equatorial Guinea ambayo imepoteza mechi zote mbili za mwanzo.



.png)
0 comments:
Post a Comment