• HABARI MPYA

    Thursday, May 29, 2014

    YANGA KUBADILISHA KATIBA POLISI JUMAPILI

    Na Nagma Said, DAR ES SALAAM
    MKUTANO Mkuu wa wanachama wa Yanga SC kufanya mabadiliko ya baadhi ya vipengele katika Katiba yao, utafanyika Jumapili wiki hii katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam kuanzia Saa 3:00 asubuhi.
    Taarifa ya Yanga SC imesema kwamba, wanachama wote hai wa klabu hiyo ndiyo wanatakiwa kufika siku hiyo.
    Marekebisho hayo yanafuatia maagizo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambao nao wamepata mwongozo kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

    Baada ya marekebisho yatakayofanyika siku hiyo, uongozi wa Yanga utapeleka Katiba hiyo TFF na kwa Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo kwa ajili ya kuhakikiwa.
    Aidha, Yanga SC imewataka wanachama wake ambao hawajalipia kadi zao hadi mwezi ujao, Juni 2014 kufanya hivyo ili wapate haki ya kuhudhuria Mkutano huo.
    Taarifa imesema malipo yote yanafayika kwenye Idara ya Fedha makao makuu ya klabu kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi saa za kazi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA KUBADILISHA KATIBA POLISI JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top