• HABARI MPYA

  Saturday, May 24, 2014

  DIEGO COSTA, RONALDO WOTE WAANZISHWA FAINALI LIGI YA MABINGWA

  Na Juma Pinto, LISBON
  MSHAMBULIAJI Diego Costa ameanzishwa katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu yake, Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid inayoanza Saa 4:45 usiku huu kwa saa za Afrika Mashariki Uwanja wa Luz mjini hapa.
  Kocha Diego Simeone amepanga karibu kikosi kile kile kilichocheza mechi ya mwisho ya msimu wa La Liga na Barcelona pamoja na Costa ambaye ni majeruhi aliyekwenda kutibiwa kwa mganga wa kienyeji Serbia wiki hii ili awahi mchezo huo.  
  Nani atabeba mwali? Kombe la Ligi ya Mabingwa likiwa uwanja wa Luz usiku huu 
  Katika mchezo huo unaochezeshwa na refa Bjorn Kuipers wa Uholanzi, upande wa Real, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema wote wameanzishwa. 
  Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Modric, Khedira, Di Maria, Bale, Benzema na Ronaldo.
  Benchi: Diego Lopez, Pepe, Marcelo, Arbeloa, Morata, Isco, Illarramendi.
  Atletico Madrid: Courtois, Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis, Raul Garcia, Gabi, Tiago, Koke, Villa na Diego Costa.
  Benchi: Aranzubia, Mario Suarez, Adrian, Rodriguez, Alderweireld, Diego na Sosa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIEGO COSTA, RONALDO WOTE WAANZISHWA FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top