• HABARI MPYA

  Wednesday, May 28, 2014

  MZEE KINESI AJITOA UCHAGUZI SIMBA SC

  Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
  JOSEPH Itang'are 'Mzee Kinesi', Kaimu Makamu Rais wa Simba, ametangaza kujitoa katika kinyang'anyiro cha kuusaka Umakamu wa Rais wa klabu hiyo katika uchaguzi mkuu wa Simba unaofanyika Juni 29, mwaka huu.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY muda mfupi uliopita jijini Dar es Salaam, Mzee Kinesi amesema amefikia uamuzi huo ili aangalia familia yake.
  "Nimeamua kujitoa katika kuwania nafasi hiyo kwa sababu nimeona kuna haja ya kuendeleza masuala ya familia, ninafikiri kuna haja kuwa karibu zaidi na familia yangu badala ya klabu ya Simba," amesema Kinesi.
  Nakupisha kijana, sikuwezi; Mzee Kinesi kushoto akiwa na Geoffrey Nyange 'Kaburu' mgombea mwingine wa Umakamu wa Rais wa Simba SC 

  Alipoulizwa pengine amesoma upepo na kuona kuna matatizo mbele ya safari, Mzee Kinesi amesema: "Uchaguzi uliopita nilikuwa wa kwanza katika wajumbe sita waliochaguliwa. Hata sasa nina watu wengi sana na mimi ndimi nitaamua nani aingie madarakani."
  Mzee Kinesi amejitoa wakati kuna sekeseke kubwa la kuengukiwa kwa Michael Wambura anayeutaka Urais wa Simba na kesho saa anawasilisha rufaa katika Shirikisho la Soka nchini (TFF) kupinga maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MZEE KINESI AJITOA UCHAGUZI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top