• HABARI MPYA

  Sunday, May 25, 2014

  DIEGO SIMEONE ALIPOTAKA KUZIPIGA NA BEKI WA REAL MADRID, KUFUNGWA NI SHIDA!

  KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone usiku wa jana alitaka kuzichapa beki wa Real Madrid Raphael Varane kama si kuamuliwa.
  Muargentina huyo alikaribia kabisa kuweka historia na Atletico Madrid kabla ya kugeuziwa kibao na wapinzani wake Real dakika za mwishoni katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuchapwa 4-1 akitoka kuongoza 1-0 hadi dakika mwisho kabla ya filimbi ya mwisho.
  Mabingwa hao wa La Liga walionekana kuwa katika nafasi ya kubeba na ndoo ya Ulaya pia baada ya bao la mapema la beki Diego Godin lililodumu hadi mwishoni kabisa wa mchezo, kabla ya Real kuzinduka.

  Kitimutimu: Simeone (wa pili kushoto) akitaka kumvaa Raphael Varane (kulia) baada ya Real kupata bao la nne

  Hata hivyo, ndoto za Atletico zilizimwa na beki Sergio Ramos aliyefunga bao la kusawazisha dakika ya mwisho na kufanya mchezo huo uongezewe dakika 30 za nyongeza.
  Bao la Ramos lilimkera kocha Simeone, ambaye alikimbia kuingoia uwanjani mwishoni mea dakika 90 kwenda kumkaripia refa Kuipers.
  Muargentina huyo alikerwa na kitendo cha refs huyo wa Uholanzi kuongeza dakika tank zilizotumiwa vizuri na timu ya Carlo Ancelotti kupata bao la kusawazisha.
  Simeone alipagawa zaidi baada ya mabao ya Gareth Bale, Marcelo na la penalti la Cristiano Ronaldo yaliyoipa ubingwa Real.
  Simeone, ambaye anafahamika kwa hasira za karibu, alipandisha jazba na kuingia uwanjani na kutaka kuvaana na Varane baada ya bao la Ronaldo.
  Tukio hilo lilifuatia wakati wa Los Blancos wanashangilia na Varane akaupiga mpira kuelekeza benchi kwa kocha huyo wa Atletico.
  Kitendo hicho cha Varane kilimkera Simeone ambaye aliupiga mpira kuurejesha uwanjani na kumquat mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kutaka kumvaa kabla ya watu kuwawahi na kuwatenganisha.
  Baada ya mechi, Simeone alifafanua akisema kwamba alikerwa na kitendo cha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kushangilia mbele ya benchi la Atletico.
  "Ni mchezaji mkubwa na ana maisha marefu mbele yake, lakini ilikuwa kero, katika 4-1 haikuwa na maana kufanya vile," alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIEGO SIMEONE ALIPOTAKA KUZIPIGA NA BEKI WA REAL MADRID, KUFUNGWA NI SHIDA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top