• HABARI MPYA

  Friday, May 23, 2014

  DAVID LUIZ AFAULU VIPIMO VYA AFYA PSG, NDIYO BYE-BYE TENA CHELSEA

  BEKI David Luiz amefaulu vipimo vya afya na kukubaliana juu ya Mkataba na Paris Saint-Germain kuelekea uhamisho wa Pauni Milioni 50 kuhamia kwa wababe hao wa Ufaransa.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatarajiwa kuwa beki ghali duniani uhamisho wake ukipiku usajili wa mabeki wawili waliokuwa wanashikilia rekodi ya wachezaji ghali wa nafasi ya ulinzi waliponunuliwa na PSG, Marquinhos na Thiago Silva.
  Wawakilishi wa PSG leo walisafiri hadi Brazil kwenda kukamilisha vipimo vya mchezaji huyo aliye kambini na timu ya wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
  Vidole mawinguni: Nyota wa Chelsea, Luiz amecheza mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo na sasa anaelekea PSG kwa dau la Pauni Milioni 50
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DAVID LUIZ AFAULU VIPIMO VYA AFYA PSG, NDIYO BYE-BYE TENA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top