• HABARI MPYA

  Saturday, May 24, 2014

  ROBBEN AITOLEA MBAVUNI MAN UNITED, ASEMA; "KUNA ASILIMIA SIFURI KUTUA OLD TRAFFORD"

  WINGA Arjen Robben amesema kuna 'asilimia sifuri' ya nafasi ya yeye kuondoka Bayern Munich kuhamia Manchester United msimu ujao.
  Nyota huyo wa Uholanzi ni miongoni mea wachezaji wall katika dada za kocha mpya wa United, Louis van Gaal anaotaja kuwasajili kutoka Bundesliga na katika timu yake ya taifa, Uholanzi.
  Lakini Robben amesema anafurahia maisha chini ya kocha Pep Guardiola Ujerumani.
  Siendi Manchester: Robben amewakata maini Manchester United na Van Gaal baada ya kusema anabaki Ujerumani
    
   "Nafasi ya kuondoka ni asilimia sifuri," amesema Robben akizungumza na gazeti la De Telegraaf la nchini mwao. "Ukweli ni kwamba, nipo katika klabu ambayo mimi na familia yang tuna wakati mzuri,".
   Robben alikuwa akizungumza katika iambi ya mazoezi ya Uholanzi nchini Ureno jana na amesema kwamba Guardiola na Van Gaal ni makocha wazuri aliowahi kufanya nao kazi.
   Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 pia amesema United imevuna dhahabu kwa kumnyakua Van Gaal, ambaye ametengewa bajeti ya Pauni Milioni 200 za usajili.
   • Blogger Comments
   • Facebook Comments

   0 comments:

   Item Reviewed: ROBBEN AITOLEA MBAVUNI MAN UNITED, ASEMA; "KUNA ASILIMIA SIFURI KUTUA OLD TRAFFORD" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

   PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

   Scroll to Top