• HABARI MPYA

    Friday, May 23, 2014

    EVRA AONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA MAN UNITED

    BEKI Patrice Evra ameongeza Mkataba wa mwaka mmoja Manchester United, klabu hiyo imethibitisha.
    Ilionekana kama Evra mwenye umri wa miaka 33 ataondoka baada ya United kuweka mezani dau la Pauni Milioni 27 kumnunua beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw.
    Lakini beki huyo aliyetua United mwaka 2006 akitokea Monaco ya nyumbani kwao, Ufaransa ameamua kuendelea na kazi hadi mwisho wa mwaka wa kwanza wa Louis van Gaal kazini.
    Anabaki: Patrice Evra ameongeza Mkataba wa mwaka mmoja Manchester United
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EVRA AONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top