• HABARI MPYA

  Sunday, May 25, 2014

  NI REAL MADRID BINGWA ULAYA, YAIFUMUA ATLETICO 4-1 URENO

  Na Juma Pinto, LISBON
  REAL Madrid ndiyo wafalme wapya wa soka Ulaya. Hiyo inafuatia kuwafunga jirani zao, Atletico Madrid mabao 4-1 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa usiku huu Uwanja wa Luz mjini hapa iliyodumu kwa dakika 120.
  Hilo linakuwa taji la kwanza kwa Real tangu mwaka 2002 na la 10 jumla baada ya awali kulibeba katika miaka ya 1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000 na 2002.
  Hii ni mara ya pili kwa Atletico Madrid kupoteza mechi katika fainali baada ya mwaka 1974 na kufungwa na Bayern Munich.
  Mkali kweli; Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga bao la nne kwa penalti
  Gareth Bale akishangilia baada ya kufunga bao la pili

  Dakika 90 zilizimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Real Madrid wakisawazisha dakika za majeruhi kwa bao la kichwa la Sergio Ramos dakika ya 90 na ushei.
  Atletico Madrid walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza bao 1-0 lililofungwa na Diego Godin kwa kichwa dakika ya 36 akiunganisha krosi kutoka upande wa kulia.
  Gareth Bale alishindwa kuokoa krosi hiyo na kipa Iker Casillas akatoka mapema langoni na kukutana na mpira uliopigwa na Godin unaelekea nyavuni. Casillas aliukimbilia mpira huo na kuuwahi kuutolea nyavuni, lakini haukutoka.
  Ikumbukwe Godin ndiye aliyefunga bao la kusawazisha katika sare ya 1-1 na Barcelona kwenye mchezo wa mwisho wa La Liga ambao uliipa Atletico ubingwa wa Hispania. 
  Mapema dakika ya tisa Atletico Madrid ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Diego Costa kuumia na kutoka nje nafasi yake ikichukuliwa na Adrian Lopez.
  Delight: Ramos celebrates his dramatic equaliser in front of the ecstatic Real Madrid supporters
  Bao la kusawazisha: Ramos akishangilia baada ya kuifunia Real Madrid bao la kusawazisha
  Relief: Casillas, who made the mistake in the first half, celebrates with Marcelo
  Ushindi bila shaka: Casillas, aliyefanya makosa yaliyoipa bao Atletico akimpongeza Marcelo baada ya kufunga bao la tatau

  Diego Costa anakuwa mchezaji wa kwanza kubadilishwa mapema zaidi katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu mwaka 1985 Mark Lawrenson wa Liverpool alipompisha Gary Gillespie dakika ya tatu.
  Mchezo ulitawaliwa na rafu nyingi Atletico wakiwachezea undava wachezaji wa Real na kufanikiwa kuwapunguza kasi na refa Bjorn Kuipers wa Uholanzi alishindwa kuidhibiti hali hiyo.
  Real ilicharuka dakika 10 za mwisho na kushambulia sana langoni mwa Atletico, hadi kufanikiwa kupata bao la kusawazisha licha ya kukosa kadhaa ya wazi.
  Katika dakika 30 za nyongeza, Gareth Bale alifunga bao la pili dakika ya 110 na Marcelo dakika ya 118 na Cristiano Ronaldo dakika ya 120 kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari.
  Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao/Marcelo dk59, Modric, Khedira/Isco dk59, Di Maria, Bale, Benzema/Morata dk79 na Ronaldo.
  Atletico Madrid: Courtois, Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis/Alderweireld dk83, Raul Garcia/Sosa dk66, Gabi, Tiago, Koke, Villa, Diego Costa/Adrian dk9.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI REAL MADRID BINGWA ULAYA, YAIFUMUA ATLETICO 4-1 URENO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top