• HABARI MPYA

  Sunday, May 25, 2014

  STARS NA MALAWI KIINGILIO BUKU TANO

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  KIINGILIO cha chini cha mechi ya kirafiki kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (Flames) itakayofanyika Jumanne (Mei 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
  Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
  Mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni ili kutoa fursa kwa washabiki wengi zaidi kuishuhudia kwa vile itakuwa ni siku ya kazi.
  Mrisho Ngassa anatarajiwa kuiongoza Stars keshokutwa 

  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili asubuhi ya siku hiyo hiyo ya mechi kutoka Tukuyu mkoani Mbeya ambapo imepiga kambi yake chini ya Kocha Mholanzi Mart Nooij.
  Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi tayari ipo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotumiwa na timu zote kama maandalizi ya mwisho kwa ajili mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON).
  Wakati Stars kwenye mechi za AFCON itarudiana na Zimbabwe jijini Harare, Flames nayo itakuwa ugenini N’djamena kukabili Chad.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STARS NA MALAWI KIINGILIO BUKU TANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top