• HABARI MPYA

    Sunday, May 25, 2014

    MUHAMMAD NAUMAN NDIYE BWANA MISULI TISHIO BONGO 2014

    Na Nagma Said, DAR ES SALAAM
    MCHEZAJI Muhammad Nauman jana ametangazwa kuwa bingwa wa michuano ya kutunisha misuli nchini katika Ukumbi wa AT. Pj uliopo Kinondoni zamani, Fin Club.
    Nauman ametangazwa mshindi baada ya kuwashinda washiriki wenzake 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini.
    Mashindano hayo yaliongozwa na mgeni na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo sambamba na Naibu Mkurugenzi wa Michezo, Juliana Yasoda.
    Mbali na Nauman, nafasi ya pili ya michuano hiyo ilikwenda kwa Mussa Mohammed huku mshindi wa tatu ni Manjohnny Luanda.
    Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga akimkabidhi Muhammad Nauman cheti cha ubingwa wa michuano ya kutunisha misuli yaliofanyika juzi katika Ukumbi wa AT. Pj uliopo kinondoni zamani Fin Club.

    Kwa ushindi huo, Nauman alifanikiwa kuondoka kwenye ukumbi huo na Sh 500,000, mshindi wa pili 400,000 huku 300,000 ikienda kwa mshindi wa tatu.
    Mbali na zawadi hizo washiriki walioingia kumi bora wote wamefanikiwa kuondoka na sh 50,000 kila mmoja.
    Washiriki hao ni Abbas Salum, Jackson Sylvester, Kayumba Ali, Mohammed Mussa, Mussa Yusuph, Ramadhani Abdallah na Mussa Midayo.
    Akizungumzia na Michuano hiyo, Mkurugenzi wa mashindano hayo, Mohammed Alli alisema mwaka huu wamechelewa kufanya maandalizi ya kutosha ila watajipanga kwa ajili ya mwakani.
    “Tumefanya mashindano hayo ila hatukujiandaa ipasavyo, ila hamasa tuliyoipata mwakani tutajipanga zaidi,”alisema
    Naye Mratibu wa michuano hiyo, Fike Willson alisema kwamba mashindano hayo ni maandalizi ya michuano ya kimataifa itakayofanyika Disemba mwaka huu.
    Alisema wamepata vijana wengi wenye uwezo, hivyo wataweza kuyarudisha mashindano hayo ambayo mara ya mwisho kufanyika ilikuwa 2002.
    Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, vijana 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUHAMMAD NAUMAN NDIYE BWANA MISULI TISHIO BONGO 2014 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top