• HABARI MPYA

  Monday, May 26, 2014

  CHELSEA WAANZA FUJO, WATAKA KUSAJILI BEKI LILIO NJIANI KUTUA MAN UNITED

  KLABU ya Chelsea imemgeukia beki Luke Shaw ambaye tayari yupo kwenye rada za Manchester United. 
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England amewakata maini Manchester City waliokuwa wanamtaka pia baada ya kuonyesha dhamira yake ya kujiunga na mahasimu, Man United kwa dau la Pauni Milioni 27. 
  Pamoja na hayo, kuzorota kwa mawasiliano juu ya dili hilo siku za karibuni kumeifanya Chelsea ijaribu bahati yake kwa mlinzi huyo. 
  Anatakiwa: Beki wa kushoto wa Southampton na England, Luke Shaw anatakiwa na Chelsea

  Southampton imekataa ofa hadi sasa kumuuza Adam Lallana na Liverpool inatakiwa kuongeza Pauni Milioni 5 kufidia malipo ya Bournemouth, wakati Dejan Lovren, Morgan Schneiderlin, Jay Rodriguez, Calum Chambers na Victor Wanyama wote wamewekwa sokoni.
  Wakati huo huo, Manchester City, wamefufua nia ya kumsajili Cole. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA WAANZA FUJO, WATAKA KUSAJILI BEKI LILIO NJIANI KUTUA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top