• HABARI MPYA

  Friday, May 30, 2014

  STARS WAFUNGIWA HOTELI HARARE, VISA VYAANZA MAPEMA

  Na Mwandishi Wetu, HARARE
  MSAFARA wa watu 30 wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars unaojumuisha wachezaji, benchi la ufundi umefungiwa vyumba vya hoteli mjini Harare Zimbabwe, ambako wapo kwa ajili ya mchezo na wenyeji kesho hatua za awali za Kombe la Mataifa ya Afrika. 
  Stars imefikia katika hoteli ya Best City Lodge mjini Harare na baada ya wachezaji kurejea kutoka mazoezini, wakanyimwa funguo za kuingia vyumbani, wakiambiwa hawajalipiwa malazi hapo.
  Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mapokezi baada ya kuzuiliwa kuingia vyumbani
  Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto na wachezaji wenzake wakiwa mapokezi

  Wakati huu wachezaji wakiwa eneo la mapekezi wameketi, viongozi wa TFF wanahaha kutatua tatizo hilo.  
  Stars itacheza na Zimbabwe Jumapili mechi ya marudiano ya hatua ya kwanza ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
  Katika mchezo wa kwanza, Tanzania ilishinda bao 1-0 wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na Jumapili Uwanja wa Taifa wa Harare, itahitaji sare ili kusonga mbele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STARS WAFUNGIWA HOTELI HARARE, VISA VYAANZA MAPEMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top