• HABARI MPYA

  Monday, May 26, 2014

  KOZI ZA UKOCHA LESENI A, B KUFANYIKA JUNI

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  KOZI ya ukocha wa mpira wa miguu kwa ajili ya Leseni A na B zinazotambuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF)  zitafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 2 mwaka huu.
  Ada kwa kozi ya Leseni A itakayoanza Julai 21 hadi 26 mwaka huu ni sh. 300,000 wakati ile ya Leseni B itakayofanyika kuanzia Juni 2 hadi 15 mwaka huu ni sh. 200,000. Maombi ya kushiriki kozi hizo yatumwe kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati kwa upande wa Zanzibar yatumwe kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kabla ya Mei 31 mwaka huu.

  Washiriki ambao watajitegemea kwa chakula watalipa ada hizo wakati wa usajili utakaofanyika Juni 1 mwaka huu kwa upande wa Leseni B na Leseni A watalipa Julai 20 mwaka huu vilevile wakati wa usajili.
  TFF itatoa malazi kwa washiriki kwenye hoteli yake iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati wakufunzi wa kozi hizo ni Sunday Kayuni na Salum Madadi ambao wanatambuliwa na CAF. Pia CAF baadaye itatuma Mkufunzi atakayetunga na kusimamia mitihani hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOZI ZA UKOCHA LESENI A, B KUFANYIKA JUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top