• HABARI MPYA

    Monday, May 26, 2014

    ATLETICO WAFUNGUKA; "HAUZWI COSTA WALA YEYOTE, HATA COURTOIS KURUDI CHELSEA KAZI IPO"

    KLABU ya Atletico Madrid itapambana kuhakikisha wachezaji wake bora na inatumai kwa umuhimu wao jatika klabu na kwa kocha wao, Diego Simeone itasaidia wakibaki.
    Kipa wa Chelsea anayecheza kwao kwa mkopo, Thibaut Courtois amezungumzia mustakabali wake baada ya kufungwa Real Madrid 4-1 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini kwa kiasi kikubwa hayuko mikononi mwa Atletico.
    "Sina mawasiliano ya moja kwa moja na Chelsea,"amesema kipa huyo mwenye umri wa miaka 22, Courtois. "Sina lolote dhidi yao. Ni kwamba nina dhamana hii na Atletico, baada ya yote nimeishi na klabu hii kwa misimu mitatu iliyopita,".
    Hauzwi; Atletico Madrid imesema haina mpango wa kumuuza Diego Costa kulia Emotional: Goalkeeper Thibaut Courtois says he has no 'emotional link' to his parent club Chelsea
    Mikono salama: Kipa Thibaut Courtois amesema hana mawasiliano ya moja kwa moja na Chelsea

    "Ikiwa nitatakiwa kurudi Chelsea tu kwa ajili ya kucheza mechi za Kombe la FA na Kombe la Ligi, nitaangalia mazingira," amesema. 
    Mtendaji Mkuu wa Atletico, Miguel Angel Gil Marin, amesema kwamba Diego Costa atauzwa iwapo tu atataka mwenyewe kuondoka. 
    Gil amesema: "Tutajaribu kuhakikisha kwamba wachezaji wore muhimu wanabaki hapa. Tumezungumza vizuri sana na Diego abaci na tunataka kutimiza ndoto hii, lakini itategemea na yeye mwenyewe,".
    "Lengo letu ni kutouza mchezaji yeyote labda yule ambaye ataomba mwenyewe kuuzwa. Kwa sababu ya mafanikio yeti katika Ligi ya Mabingwa, tuna fedha maana yake hatuhitaji kuuza mchezaji,"amesema. 
    Wanted: Koke (above) and Filipe Luis (below) are also attracting interest from the Premier League
    Wanatakiwa: Koke (juu) na Filipe Luis (chini) nap pia wanamuliwa na klabu za Ligi Kuu ya England
    Atletico defender Filipe Luis
    Kiungo Koke na beki wa kushoto, Filipe Luis ni wachezaji winging wanaozitoa udenda klabu za Ligi Kuu ya England. Lakini Koke ni kipenzi cha klabu hiyo na Filipe Luis na rafiki wa kocha Simeone, hali ambayo inaweza kuwafanya wabaki. 
    Simeone amesema: "Tutakuwa na mapumziko ya kutosha, kuangalia Kombe la Dunia na kisha tutarejea kutetea ubingwa wetu wa Ligi,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ATLETICO WAFUNGUKA; "HAUZWI COSTA WALA YEYOTE, HATA COURTOIS KURUDI CHELSEA KAZI IPO" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top