• HABARI MPYA

  Saturday, May 24, 2014

  MBEYA CITY YAANZA VYEMA MICHUANO MIPYA CECAFA, WAPIGA MTU TATU, WAUWAJI MWAGANE YEYA, PUAL NONGA NA MTU MPYA THEMI FELIX KUTOKA KAGERA

  Na Rodgers Mulindwa, KHARTOUM
  WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano mipya ya klabu ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) iitwayo Nile Basin, Mbeya City wameanza vizuri leo baada ya kuifunga mabao 3-2 Academie Tchite ya Burundi mjini Khartoum, Sudan.
  Mabao ya Mbeya City katika mchezo huo wa Kundi B yamefungwa na Paul Nonga dakika ya 15, mshambuliaji mpya Themi Felix kutoka Kagera Sugar dakika ya 27 na Mwagane Yeya dakika ya 37. Mabao ya timu ya Burundi yamefungwa na Rashid Patient dakika ya 10 na Munirakiza Cedric dakika ya 68.
  Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia moja ya mabao yao leo

  Ushindi huo unawaweka Mbeya City katika nafasi nzuri ya kutinga Robo Fainali ya michuano hiyo.
  Mapema katika mechi za ufunguzi jana, mabao saba yalitinga nyavuni, Victoria University ya Uganda ikiilaza 1-0 Malakia ya Sudan Kusini, El-Merreikh waliichapa 3-0 Polisi ya Zanzibar na El-Shandi waliilaza 2-1 Dkhill ya Djibouti.
  Michuano hiyo inashirikisha mabingwa wa Kombe la FA na washindi wa pili wa Ligi Kuu wa nchi wanachama wa CECAFA. Mbeya City imechukua nafasi ya Azam FC, washindi wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita, ambao wamejitoa.
  Simba SC ambao wangechukua nafasi ya Azam, wakati taarifa inakuja ya kufanyika kwa mara ya kwanza michuano hiyo, walikuwa wamekwishavunja kambi na wachezaji wao wote walikuwa wameruhusiwa likizo.
  Paul Nonga wa Mbeya City akipambana na Kabeya Kalala wa Academie Tchite aliyelala kuondosha mpira kwenye hatari
  Deogratius Julius wa Mbeya City akipambana na Dieudonne Issa wa Academie Tchite
  Mwagane Yeya wa Mbeya City akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Academie Tchite
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAANZA VYEMA MICHUANO MIPYA CECAFA, WAPIGA MTU TATU, WAUWAJI MWAGANE YEYA, PUAL NONGA NA MTU MPYA THEMI FELIX KUTOKA KAGERA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top