• HABARI MPYA

  Sunday, May 25, 2014

  SAMATTA AING’ARISHA TP MAZEMBE LIGI YA MABINGWA, YAIBUTUA TENA AS VITA 1-0

  Na Prince Akbar, LUBUMBASHI
  BAO pekee la Mbwana Ally Samatta jioni ya leo limeipa ushindi wa kwanza TP Mazembe katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita uliofanyika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Samatta ambaye DRC ni maarufu kama Sama Goal mbele ya mashabiki wa timu yake, alifunga bao hilo pekee dakika ya 62 na kuifanya Mazembe ifufue matumaini ya kutwaa Kombe la tano la michuano hiyo. 

  AS Vita ya Lubumbashi, DRC inafungwa kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu na ndugu zao hao, baada ya awali kufungwa katika mechi zote za Ligi Kuu ya nchi hiyo.
  Samatta alimpisha Jonas Sakuwaha dakika ya 82, wakati mshambuliaji mwingine Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu alitokea benchi dakika ya 67 kwenda kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.  
  Mazembe sasa ina pointi tatu sawa na AS Vita iliyoifunga Zamalek 2-1 katika mchezo wa kwanza wiki ambayo akina Samatta walilala 1-0 mbele ya El Hilal nchini Sudan.
  Matokeo ya leo yanafanya kila timu katika kundi hilo iwe imefungwa mechi moja na kushinda mechi moja, baada ya El Hilal pia kufungwa 2-1 na Zamalek jana. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AING’ARISHA TP MAZEMBE LIGI YA MABINGWA, YAIBUTUA TENA AS VITA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top