• HABARI MPYA

    Saturday, May 24, 2014

    NKANA YASHIKWA 1-1 NYUMBANI NA SEWE, ASEC, COTONSPORT NAZO ZABANWA BARAZANI KWAO

    Na Mwandishi Wetu, KITWE
    NKANA FC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Sewe Sport de San Pedro ya Ivory Coast katika mchezo wa Kundi B Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Nkana mjini Kitwe, Zambia.
    Wageni walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Roger Assale kabla ya Ronald Kampamba kuwasawazishia wenyeji dakika ya 54.

    Katika mechi nyingine za Kundi A michuano hiyo zilizochezwa leo, Cotonsport ya Cameroon imelazimishwa sare ya bila kufungana na Real Bamako sawa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast iliyotoka 0-0 na Leopards FC ya Kongo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NKANA YASHIKWA 1-1 NYUMBANI NA SEWE, ASEC, COTONSPORT NAZO ZABANWA BARAZANI KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top