• HABARI MPYA

    Saturday, May 24, 2014

    TIKETI ZAZUA MAANDAMANO LISBON, YAKADIRIWA MASHABIKI 30,000 HAWAJAZIPATA

    Na Juma Pinto, LISBON
    MASHABIKI wa soka kuoka Hispania waliokuja kuzisapoti timu zao Real Madrid na Atletico Madrid wamejimwaga mitaani kuandamana baada ya kukosa tiketi za kushuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa Uwanja wa Luz baadaye leo baina ya timu hizo.
    Inasadikiwa zaidi ya mashabiki 30,000 hawajapata tiketi na wameendelea kujimwaga mitaani wakiwa na jezi, bendera na skau za timu zao pamoja na mavuvuzela.
    Real na Atletico zinatakuwa katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa leo Uwanja wa Luz mjini hapa, huo ukiwa ni mchezo wa kuhitimisha msimu wa 59 wa michuano hiyo mikubwa zaidi ya klabu Ulaya na msimu wa 22 tangu michuano hiyo ianze kutumia jina hilo kutoka Klabu Bingwa ya Ulaya.
    Tatizo: Mashabiki wakiwa na mabango wakiandamana mitaa ya Lisbon baada ya kukosa tiketi
    Watanzania wamezipata kiulaini; Mgombea nafasi ya Ujumbe katika uchaguzi Mkuu wa Simba SC mwezi ujao, Juma Abbas Pinto kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habra za Michezo Tanzania (TASWA) akiwa na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kimataifa wa Real Madrid, Rayco Garcia kulia na Msemaji wa makampuni ya TSN, Dennis Ssebo mjini Lisbon pamoja na tiketi zao
    Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo kukutanisha timu kutoka Jiji moja, Madrid.
    Bingwa wa michuano hiyo anatarajiwa kujinyakulia kitita cha Euro Milioni 10.5 na mshindi wa pili Euro Milioni 6.5 wakati timu zilizotolewa katika Nusu Fainali, Beyern na Barcelona kila moja itapata Euro Milioni 4.9.
    UEFA pia hutoa Euro Miloni 2.1 kwa kila timu inayofuzu kwenye Raundi ya awali ya michuano hiyo, Euro Milioni 8.6 kwa zinazoingia hatua ya makundi, wakati timu inayoshinda mechi katika hatua hiyo inapata Euro Milioni 1 na sare Euro 500,000. 
    Timu zinazongia kwenye hatua ya 16 Bora inapata Euro Milioni 3.5 wakati kwa zinazofuzu Robo Fainali zinapata Euro Milioni 3.9. 
    Wakati Real ina mataji tisa iliyoyatwaa misimu ya 
    1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000 na 2002 pamoja na kushika nafasi ya pili mara tatu 1962, 1964 na 1981, Atletico Madrid iliingia fainali mara moja tu mwaka 1974 na kufungwa na Bayern Munich.
    Nyota wa Real, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale waliokuwa majeruhi wote wamepona na wamekuja na timu yao Lisbon tayari kwa kuipigania kapata taji la 10 la michuaho hiyo.
    Mshambuliaji tegemeo wa Atletico Madrid, Diego Costa aliyekuwa majeruhi jana ameanza mazoezi mepesi baada ya mapema wiki hii alipelekwa Serbia kutibiwa na mganga wa kienyeji ili aweze kupona haraka na kucheza.     
    Atletico tayari wameshinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania msimu huu ikiwazidi kete vigogo wa nchi hiyo Barcelona siku ya mwisho walipotoa nao sare ya 1-1 na Real baada ya kukosa taji la La Liga watakuwa wanajaribu kurejesha heshima katika Ligi ya Mabingwa.  
    Tangu juzi, Jiji la Lisbon limetawaliwa na shamrashamra za mashabiki wa Real na Atletico waliosafiri kutoka Madrid kuja kuzisapoti timu zao.
    Gwiji wa zamani wa Real, Mreno Luis Figo ndiye balozi wa mchezo huo ambaye baadaye anatarajiwa kuwamo katika kikosi cha magwiji wa timu hiyo kitakachofanya ziara Tanzania Agosti mwaka huu.
    Madrid invasion: Real and Atletico fans have arrived in Lisbon ahead of the Champions League final on Saturday
    Mashabiki wa Atletico Madrid wakiwa mitaa ya LisbonCraze: Real fans take a selfie in the streets while having a drink in the city
    Vimwana: Mashabiki wa Real wakijipiga picha mitaa ya Lisobn
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIKETI ZAZUA MAANDAMANO LISBON, YAKADIRIWA MASHABIKI 30,000 HAWAJAZIPATA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top