• HABARI MPYA

  Thursday, May 29, 2014

  MBEYA CITY KUCHEZA NA WAKALI WA UGANDA ROBO FAINALI MICHUANO MIPYA YA CECAFA

  Na Rogers Mulindwa, KHARTOUM
  MBEYA City itamenyana na timu tishio kutoka Uganda, Victory University katika Robo Fainali ya michuano ya Nile Basin Jumamosi ya Mei 31, Uwanja wa Khartoum Sudan.
  Hiyo itakuwa robo Fainali ya kwanza siku hiyo itakayoanza Saa 11:30 jioni na kufuatia na mchezo mwingine kati ya wenyeji El Ahli Shandi dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini.
  Awali, kesho zitachezwa Robo Fainali mbili za kwanza kati ya AFC Leopards ya Kenya na Defence  ya Ethiopia Saa 11:30 kabla ya wenyeji El Merreikh kuumana na Academie Tchite ya Burundi.
  Kazi wanayo; Mbeya City watamenyana na Victory University Jumamosi katika Robo Fainali michuano ya Nile Basin 

  Mbeya City ilitinga Robo Fainali za michuano ya Nile Basin inayoendelea nchini Sudan kufuatia sare ya bila kufungana na Enticelles ya Rwanda usiku wa jana Uwanja wa Khartoum.
  Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City imalize na pointi nne baada ya mechi tatu, ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya AFC Leopards ya Kenya walioongoza kundi kwa pointi zao tisa.
  Enticelles imemaliza nafasi ya pili kwa pointi zake mbili na Academie Tchite ya Burudi imemaliza mkiani mwa Kundi B kwa pointi moja iliyovuna kwenye sare na timu ya Rwanda.
  Michuano hii inayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA au washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), inafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, Sudan wakiwa wenyeji wa kwanza.
  CECAFA imeanzisha mashindano hayo kwa lengo la kuongeza changamoto kwa klabu za ukanda wake. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY KUCHEZA NA WAKALI WA UGANDA ROBO FAINALI MICHUANO MIPYA YA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top