• HABARI MPYA

    Saturday, May 31, 2014

    ZAMBIA WAENDA MAREKANI JUNI 3 BILA MWEENE

    Na Mahmoud Zubeiry, LUSAKA
    TIMU ya soka ya taifa ya Zambia, itaondoka Lusaka Juni 3, kwenda Marekani kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na Japan Juni 6 mjini Florida.
    Wachezaji wote wa kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa zamani wa Afrika wamekusanyika hapa kwa mazoezi makali, kasoro kipa wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Kennedy Mweene ambaye ni majeruhi.
    Mweene aliumia nyama akiichezea Sundowns mchezo wa kirafiki nchini Namibia na kocha Patrice Beaumelle amesema hajataka kumharakisha kurudi uwanjani, kuhofia ataumia zaidi.
    Atakosekana; Kipa Kennedy Mweene atakosa safari ya Marekani na timu yake ya taifa 

    Na sasa vita ya kuwania kurithi nafasi ya mlango mlango huyo inahamia kwa kipa wa Nchanga Rangers, Toaster Nsabata na Joshua Titima wa Power Dynamos, zote za hapa.
    Wakati huo huo, kiungo wa Zanaco, Isaac Chansa anatarajiwa kurejea kuichezea Chipolopolo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 nchini Gabon kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika.
    Mchezaji mwenzake wa klabu hiyo, winga Roderick Kabwe atakosa pia nsafari ya Marekani kutokana na msiba wa mama yake mzazi mwishoni mwa wiki.
    Wachezaji wawili wameongezwa akiwemo kiungo wa Power Dynamos na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Lubambo Musonda na beki wa Green Buffaloes, Adrian Chama katika kikosi cha wachezaji 22 watakaokwenda ziara hiyo.
    Kikosi kamili ni, makipa; Toaster Nsabata (Nchanga Rangers) na Joshua Titima (Power Dynamos), mabeki; Adrian Chama (Green Buffaloes), Jimmy Chisenga (Red Arrows), Stoppila Sunzu (Sochaux, Ufaransa), Hichani Himonde (Mamelodi Sundowns, Afrika Kusini), Joseph Musonda (Golden Arrows, Afrika Kusini), Emmanuel Mbola (Hapoel, Israel) na George Chilufya (Nchanga Rangers).
    Viungo ni Kondwani Mtonga, Justin Zulu (wote Zesco United), Isaac Chansa (Zanaco) Nathan Sinkala (TP Mazembe, DRC), Chisamba Lungu (FC Ural, Urusi), Felix Katongo (Green Buffaloes), Lubambo Musonda na Kennedy Mudenda (wote Power Dynamos).
    Washambuliaji ni Christopher Katongo (huru), Jacob Mulenga (huru), Emmanuel Mayuka (Southampton, England), Moses Phiri (wote Zanaco) na James Chamanga (Liaoning Whowhin, China).

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAMBIA WAENDA MAREKANI JUNI 3 BILA MWEENE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top