• HABARI MPYA

  Friday, May 30, 2014

  SERIKALI YAMUONYA MALINZI AACHANE NA MPANGO WA KUBADILI JINA LA TAIFA STARS

  Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM
  SERIKALI imelitaka Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuachana na mpango wa kubadilisha jina la timu ya taifa (Taifa Stars) badala yake ijikite katika kuboresha kikosi cha timu hiyo.
  Akijibu maswali ya wabunge leo asubuhi Bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (pichani chini), amesema hakuna haja ya kubadili jina hilo kwa kuwa kufanya hivyo serikali haioni kama kutakuwa na mantiki.

  "Tumepokea maoni ya TFF kutaka kubadili jezi za timu ya taifa kwa kuwa rangi ya bluu kwenye TV inaleta matatizo. Pia wamependekeza kubadili jina la timu ya taifa. Serikali inaona hakuna haja ya kubadili jina badala yake wajikite katika kubadili mchezo wenyewe," amesema Nkamia.
  Mapema mwezi huu, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema jijini Dar es Salaam kuwa watakusanya maoni ya Watanzania kupata jina jipya la timu ya taifa na aina ya jezi ambazo timu hiyo itakuwa inavaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERIKALI YAMUONYA MALINZI AACHANE NA MPANGO WA KUBADILI JINA LA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top