• HABARI MPYA

  Thursday, May 29, 2014

  SIRI NZITO YA RONALDO YAFICHUKA, JAMAA MJANJA SANA KUMBE

  NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo alivua jezi yake na kushangilia kama mtunisha misuli baada ya kufunga bao la mwisho katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Atletico Madrid kwenye fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya wiki iliyopita, kwa sababu maalum.
  Taarifa nchini Hispania zinasema kwamba, mwanasoka huyo bora wa alivua jezi kwa sababu alijua alikuwa anarekodiwa picha za filamu yake.
  Mtreno huyo alifunga kwa penalti dakika za mwisho kabisa za muds wa nyongeza Uwanja wa Luz mini Lisbon, Ureno na kushangilia kwa kuvua jezi kuonyesha misuli yake.
  Ushangiliaji wake haukuendana na aina ya bao alilofunga, kwanza timu ilikuwa imekwishashinda na taarira zinasema Ronaldo alijua kulikuwa kuna kamare maalum zinamrekodi ushangiliaji wake.
  Glory: The Portuguese superstar lifts the Champions League trophy at the Stadium of Light
  Bingwa: Supa staa wa Ureno akiinua Kombe la Ligi ya Mabigwa Uwanja wa Luz

  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester Unitedanatoa kitu kinaitwa 'Ronaldo' ili kupromoti bidhaa yake.
  Aliisaidia Real Madrid kutwaa taji la 10 la Ulaya mjini Lisbon wikiendi iliyopita ikitoka nyuma kwa bao 1-0 hadi dakika ya 90 na usher na kuishinda 4-1 baada ya dakika 120.
  Kwake, hilo lilikuwa taji la pili la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya awali Ronaldo kushinda taji hilo akiwa na Manchester United mwaka 2008.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIRI NZITO YA RONALDO YAFICHUKA, JAMAA MJANJA SANA KUMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top