• HABARI MPYA

  Tuesday, May 27, 2014

  MUSSA MUDDE AITEKETEZA MBEYA CITY SUDAN

  Na Rodgers Mulindwa, KHARTOUM
  MBEYA City imefungwa mabao 2-1 AFC Leopard ya Kenya katika mchezo wa Kundi B michuano ya Nile Basin uliofanyika kwenye Uwanja Khartoum, Sudan.
  Mabao yaliyozamisha Mbeya City katika mchezo wa mashindano hayo mapya ya Baraza la Soka la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inayofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu yamefungwa na kiungo wa zamani wa Simba SC Mganda Mussa Mudde na Mkenya Paul Were.
  Bao la Mbeya City limefungwa na kiungo Deus Kaseke na sasa Leopard inaendelea kuishi kileleni mwa Kundi B kwa kufikisha pointi sita, wakati Mbeya City yenye pointi tatu inabaki nafasi ya pili.
  Mussa Mudde katikati waliochuchumaa katika kikosi cha Leopard kilichoifunga Mbeya City 2-1 leo

  Mchezo huo wa michuano inayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA na washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama wa CECAFA, ulichezeshwa na refa Khalil Walida aliyesaidiwa na Mohammed Abdallah wote wa Sudan na Bogoreh Farhan wa Djibouti.
  Mbeya City; David Burhan, Mwagane Yeya, Hamad Kibopile, Deo Julius, Yohanna Morris, Antohny Matogolo, Deus Kaseke, Steven Mazanda, Paul Nonga, John Kabanda na Themis Felix.
  AFC Leopard; Patrick Matasi, Paul Were, Edwin Wafula, Eric Masika, Joseph Shikokoti, Mussa Mudde, Austin Ikenne, Juma Abdallah, Jackson Saleh, Benard Mangoli na Noah Wafula.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUSSA MUDDE AITEKETEZA MBEYA CITY SUDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top