• HABARI MPYA

  Wednesday, May 28, 2014

  TIMU YA NOOIJ YABEBA UBINGWA ETHIOPIA

  Na Mwandishi Wetu, ADDIS ABABA
  KLABU ya Saint George imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Ethiopia msimu wa 2013-2014  ikiwa na mechi tano mkononi baada ya Jumatatu kuifunga Sidama Coffee bao Uwanja wa 1-0 Yirgalem.
  Hilo linakuwa taji la rekodi la 26 kwa ‘Sanjaw’ au ‘Kidus Giorgis’ majina ya utani yanayotokana na mizuka ya mashabiki wake, wakirejesha taji walilopokonywa na Dedebit msimu uliopita.
  Mabingwa wa kihistoria; St George wakiwa na Kombe lao baada ya kukabidhiwa Jumatatu usiku

  Nyota chipukizi, Fitsum Gebremariam ambaye amekuwa tegemeo la mabao, akiifungia timu hiyo mabao yote muhimu, alifunga bao hilo pekee kipindi cha pili.
  ‘Kidus Giorgis’ hadi sasa imeshinda mechi 19 kati ya 21 ilizocheza na kuvuna pointi 58, 20 zaidi ya Ethiopia Bunna iliyo katika nafasi ya pili, wakati Dedebit inashika nafasi ya saba kwa pointi zake 27.
  Kocha mpya wa Tanzania, Mholanzi Mart Nooij ana mchango mkubwa katika ubingwa huo, kwani ndiye aliyekuwa na timu hiyo tangu mwanzo wa msimu kabla ya kuiacha mwezi uliopita kufuata ajira mpya Taifa Stars.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA NOOIJ YABEBA UBINGWA ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top