• HABARI MPYA

  Saturday, May 24, 2014

  RONALDINHO ALIGEUZA 'GESTI' JUMBA LAKE BAADA YA KUTEMWA KOMBE LA DUNIA

  BAADA ya kutemwa kwenye kikosi cha kocha Luiz Felipe Scolari cha Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia, Ronaldinho ameibuka na marina mengine ya kutengeneza fedha kupitia michuano ya mwaka huu.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona ameamua kupangisha jumbo lake la kifahari liliopo Rio de Janeiro kwa gharama za Pauni 9,120 kwa siku, ili kuwapa mashabiki fursa ya kuishi kwenye mjengo wa kifahari wa gwiji huyo wa Brazil.
  Ronaldinho ameposti kwenye Twitter kuthibitisha kwamba jumba lake lenye vyumba vitano vya kulala linapangishwa kupitia Airbnb.com wakati wa Kombe la Dunia mwaka huu.
  Ametemwa: Ronaldinho anapangisha jumba lake la Rio baada ya kuachwa kwenye kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia
  Home sweet home: Ronaldinho is charging over £9,000 per night for his five bedroom house
  Mjengo wenyewe ni huu: Ronaldinho anatoza Pauni 9,000 kwa usiku mmoja katika jumba lake lenye vyumba vitano vya kulala
  Memories: A painting of Ronaldinho during his AC Milan days hangs on the wall of the living room
  Kumbukumbu: Mchoro wa picha ya Ronaldinho wakati anacheza AC Milan ukiwa kwenye chumba cha kupumzikia
  Comfy: People have the chance to sleep in the Brazilian star's bed
  Kwa usingizi mnono: Watu wanaweza kupata fursa ya kulala kwenye kitanda cha nyota huyo wa Brazil
  Chill out: The 34-year-old's house also features a Zen room for relaxation
  Nyumba ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 pia ina chumba cha Zen kwa kupumzikia

  Nyota huyo wa Atletico Mineiro ameandika: "Hii ni kwa yeyote ambaye anaona anaweza kupanga nyumba yangu Airbnb! jiachie katika mjengo wa #CasaR10'Ronaldinho's property, ambao pia una vyumba sita vya kulala, upo ndani ya geti mjini Rio eneo la Barra da Tijuca.
  Yeyote anayeweza kupanga katika mjengo huo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ague kwamba una kitu ikiwemo sauna, barbeue, a cellar na friji la bia.
  Ronaldinho aliyechezea pia PSG na AC Milan, amelipendezesha jumba hilo kwa kuweka michoro ya picha zake mbalimbali na mtu anayetaka kupanga anatakiwa kutoa malipo ya awali ya Pauni 600, lakini hairuhusiwi kuvuta sigara ndani, labda nje ya nyumba na kutakuwa na timu maalum ya watu wa kuhudumia wageni.
  Water features: Ronaldinho's house comes with a swimming pool and sauna
  Mjengo wa Ronaldinho pia una bwawa la kuogelea na sauna
  Colourful character: The Atletico Mineiro forward has a number of paintings of himself
  Mshambuliaji huyo wa Atletico Mineiro ameweka michoro ya picha zake kadhaa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDINHO ALIGEUZA 'GESTI' JUMBA LAKE BAADA YA KUTEMWA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top