• HABARI MPYA

  Sunday, May 25, 2014

  NGORONGORO YAFUMULIWA 4-1 NIGERIA HADI AIBU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania imefungwa mabao 4-1 jana na wenyeji Nigeria katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Senegal.
  Kwa matokeo hayo, kikosi cha John Simkoko kimetolewa kwa jumla ya mabao 6-1 baada ya awali kufungwa pia 2-0 nyumbani Dar es Salaam. 

  Katika mechi nyingine ya jana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilifuzu pia baada ya kuifunga mabao 2-0 Malawi na kufanya ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGORONGORO YAFUMULIWA 4-1 NIGERIA HADI AIBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top